TPHPA Yaendeleza Ubabe Katika Mashindano ya SHIMMUTA Northern Zone

 




TPHPA - Arusha

Timu ya Mpira wa Miguu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuonyesha ubabe katika Mashindano ya SHIMMUTA northern zone, baada ya kuifunga timu ya Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC) kwa magoli mawili (2) bila kuruhusu goli lolote (0). Mchezo huu uliochezwa leo, Oktoba 10, 2024, katika viwanja vya Chuo cha Nelson Mandela, umekuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki na wapenzi wa michezo.


TPHPA, ikiwa na ari na nguvu kubwa, ilionyesha uwezo wa hali ya juu uwanjani, huku ikicheza kwa ushirikiano mzuri na mbinu sahihi. Magoli mawili yaliyowekwa na timu hiyo yanathibitisha kuwa wamejizatiti vizuri kuelekea mashindano makubwa yajayo.


Michezo hii inatekelezwa kama sehemu ya maandalizi ya kushiriki katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) 2024, yatakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu mkoani Tanga. Timu zote zinajitahidi kujiondoa na kujenga uwezo wa ushindani, na TPHPA inaonekana kuwa katika njia sahihi kuelekea mafanikio.


Mashindano ya SHIMMUTA ni fursa muhimu kwa mashirika mbalimbali kukuza michezo na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi. TPHPA inatarajiwa kuingia kwenye mashindano haya ikiwa na nguvu na motisha ya kushinda, wakitafuta kuleta taji nyumbani. Wapenzi wa timu hii wanatarajia kuona matokeo mazuri zaidi katika mechi zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Apokea Makombe 6 yaliyopatikana Katika Mashindano ya Mei Mosi na SHIMMUTA 2024