TPHPA YAPEWA ENEO LA KUJENGA OFISI WILAYA YA GAIRO,DC MAKAME ASEMA WANAFANYA KAZI KUBWA
TPHPA - Gairo
Hayo yamejiri 9 Oktoba katika Viwanja vya shule ya Gairo A katika maonyesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024, msimu wa tatu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mh.Jabiri Makame ametoa eneo kwa TPHPA kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika Wilaya hiyo ili kuendelea kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakulima Wilayani humo na maeneo ya karibu.
"Nafarijika sana na jinsi Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu inavyojikita katika kutekeleza majukumu yake hapa Tanzania hasa katika kutatua matatizo kwa wakulima ikiwepo kuokoa mazao kutokana magonjwa na wadudu waaribifu, pia udhibiti baa la panya na ndege waaribifu jamii Kweleakwelea katika mashamba bila kusahau elimu kwa wakulima na wafanyabiashara wa Viuatilifu kuhusu matumizi salama na sahihi ya viuatilifu kwa lengo la kulinda afya ya binadamu, wanyama na mazingira"alisema Mh.Makame
Akizungumzia kuhusu eneo la ofisi Mh.Jabir Makame amesema wanatoa eneo bure kwa ajili ya Mamlaka hii ili waweze kuwafikia wakulima kwa urahisi Wilayani Gairo na maeneo ya jirani, haswa ukizingatia Gairo ni eneo la kimkaati katika uzalishaji wa chakula nchini,kulinda usalama wa chakula tunachozalisha ni kipaumbele cha TPHPA na utekelezaji wa ajenda 10/30.
Nae Kaimu Meneja wa kanda ya Mashariki Dkt.Mahamudu M.Sasamalo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Joseph C. Ndunguru akizungumzia swala hilo ametoa shukrani za dhati kwa Mh.Makame kwa ukarimu huo na kutambua juhudi za TPHPA na kuona umuhimu wa kukabidhiwa eneo ili kujenga ofisi ambayo itakuwa ni msaada mkubwa sana katika kurahisisha huduma zitolewazo na TPHPA Wilayani humo na maeneo ya karibu na Wilaya hiyo, na wanasubiri kwa hamu taratibu za kiofisi kwa ajili ya makabidhiano
TPHPA AFYA YA MIMEA,AFYA YA MIMEA TPHPA
Comments
Post a Comment