WAKULIMA NA WADAU WENGINE WA KILIMO WAPATA ELIMU JUU YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU
TPHPA - Babati
Wakati maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani yakiwa yanaendelea mjini Babati, wataalamu kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wameweza kuwapatia wakulima elimu mahususi kuhusu matumizi Sahihi na Salama ya Viuatilifu kwenye kipindi maalum kilichoandaliwa na mamlaka ya udhibiti wa Mbolea.
Bw. Christian Maige ambaye ni mtaalamu kutoka TPHPA, aliweza kushiriki kuwaelekeza wakulima kuhusu aina za viuatilifu na jinsi ya kuvitumia kiusahihi kutokana na aina ya kisumbufu kinachotakiwa kudhibitiwa, aina mbalimbali za nozeli na matumizi yake, wakati sahihi wa kunyunyizia kiuatilifu shambani na pia namna ya kujikinga dhidi ya athari za viuatilifu kwa kuvaa mavazi kinga sahihi.
Mafunzo haya yalijumuisha wataalamu mbalimbali kutoka taasisi za Kudhibiti Mbolea, taasisi za kifedha ambapo waliweza kuzungumzia fursa za mikopo kwa wakulima pamoja na wauzaji wa pembejeo za kilimo.
Washiriki waliweza kutoa maoni yao na kupongeza Mamlaka kwa juhudi wanazozifanya katika kutoa elimu kuhusu matumizi ya viuatilifu kwani elimu hii inawasaidia sana pindi wanapotumia viuatilifu shambani.
Comments
Post a Comment