MCC Wahidi Kuimarisha Ushirikiano na TPHPA Kaimarisha Masoko ya Mazao Yetu Nje ya Nchi










Wataalamu elekezi kutoka Millennium Challenge Corporation (MCC) leo walifanya ziara katika makao makuu ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na  Viuatilifu  Tanzania (TPHPA), ambapo walifanya majadiliano na wataalamu wa mamlaka hiyo kwa lengo la kuelewa shughuli zinazofanyika na kuoanisha na programu ya MCC Threshold.

Lengo kuu la majadiliano haya lilikuwa kubaini maeneo ya ushirikiano, hasa katika sekta ya uwezeshaji masoko (trade facilitation), ambapo walijadili mbinu za kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao ya Tanzania nje ya nchi.

Baada ya majadiliano, wageni walifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Mamlaka, ikiwemo Kituo cha Intelijensia ya Usalama wa Afya ya Mimea, Maabara ya Uchambuzi wa Masalia Viuatilifu na Maabara ya Kuhakiki Ubora wa Viuatilifu.

Wataalamu hao kutoka MCC walishukuru kwa ushirikiano walioupata na kujibu maswali yote waliyokuwa nayo, na kuahidi kuendeleza mashirikiano baina ya pande hizi. Majadiliano hayo yamefanyika leo, tarehe 19 Novemba 2024, katika makao makuu ya Mamlaka yaliyopo Ngaramtoni, Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu