Sekunde 28 zatosha kuifanya TPHPA kuwa bingwa Mchezo Wa Magunia Wanawake SHIMMUTA 2024









Bi. Rhoda Simon aongoza mbio za Magunia Wanawake hivyo kuwa bingwa Katika Mbio za Magunia Wanawake katika Mashindano ya  Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi SHIMMUTA -TANGA


Novemba 21, 2024 – Bi. Rhoda Simon ambaye ni Mfanyakazi wa Mamlaka (TPHPA) amekuwa bingwa kwakuwa mshindi wa kwanza katika mbio za magunia Wanawake zilizofanyika leo, katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi. Ambapo alifanikiwa kumaliza mbio hizo kwa muda wa sekunde 28, na hivyo kutwaa taji la ubingwa wa Mbio za magunia, ambazo zilijumuisha washiriki 36 kutoka taasisi na mashirika mbalimbali, zilifanyika kwenye uwanja wa michezo Sekondari ya Tanga


Bi. Rhoda Simon alionyesha umahiri mkubwa, akiwaacha nyuma washindani wake kwa kutumia mbinu bora na kasi ya kipekee, na hivyo kushinda kwakuwa wakwanza katika mashindano haya yenye ushindani mkubwa.


Mashindano ya mwaka huu yalishirikisha mashirika na taasisi 91 kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na yamejulikana kwa kuleta umoja na kuimarisha afya bora miongoni mwa wafanyakazi wa mashirika hayo.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu