UGUNDUZI VIUATILIFU HALALI KIZUNGUZUNGU KWA WAKULIMA,TPHPA YAWAPA MBINU KUEPUKA UBAMBIKWAJI






TPHPA imeendelea kutoa elimu kwa Wakulima ,Wafanyabiashara wa Viuatilifu,Maafisa Ugani Mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo tarehe 18 mpaka 23 novemba  wapo Mkoani Katavi kutoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, pamoja na mada zingine Washiriki wamepewa mbinu sahihi za kugundua iwapo kiatilifu anachotaka kununua ni halali au feki.

Akizungumza Mkufunzi kutoka TPHPA ndugu Ernaus Mwinuka amesema ni muhimu kila Mkulima kuhakikisha anakuwa na uelewa wa kutosha katika kugundua kiuatilifu ambacho ni halali na kisicho na mashaka ili kuepuka kuharibu mimea jambo ambalo linalopelekea hasara kubwa kutokana na uharibifu unaotokea baada ya kutumia kiuatilifu kisicho na sifa.

Akiongelea mambo ya kuzingatia wakati wa ununuzi wa kiuatilifu  ndugu   Mwinuka amesema mnunuzi anatakiwa kuangalia taarifa za usajili kutoka Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu ,lakini pia aangalie taarifa za mwisho wa matumizi ya kiuatilifu husika,iwapo kiuatilifu kitakuwa hakina taarifa za usajili kuna uwezekano kikawa hakipo kihalali na hakijathibitishwa wala kupitishwa na mamlaka husika.

Kwa Mkoa wa Katavi Mafunzo haya yamekuwa na mwitikio mkubwa na hamasa ambapo washiriki wameitaka Mamlaka kuyaleta mafunzo haya mara kwa mara kwani mahitaji ni makubwa ili wadau wengi waweze kuelimika zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu