WAFANYABIASHARA WA VIUATILIFU MKOANI KATAVI WATAKIWA KURASIMISHA BIASHARA ZAO.






Hayo yamejiri wakati wa kufunga mafunzo ya matumizi sahihi ya Viuatilifu kwa Wafanyabiashara na Wakulima Mkoani Katavi ambapo Mgeni rasmi Kaimu RAS wa Mkoa wa Katavi ndg.Florence Lungwa amewataka Wafanyabiashara wa viuatilifu kurasimisha biashara zao kwa kukata vibali na kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwepo kupata mafunzo ili kuwa huru na biashara zao kwani kufuata taratbu kutawafanya wajiamini na kuwa huru katika kazi zao,lakini pia itakuwa wamefuata matakwa ya kisheria.


Sambamba na hilo ndugu Florence  Lungwa amewataka kwenda kurekebisha makosa mbali mbali yaliokuwa yakifanyika au ambayo yangefanyika, "Mkarekebishe kulingana na taratibu mlizoelekezwa, msiruhusu watoto wadogo kuuza viuatilifu, msipimie watu viuatilifu, msichanganye viuatilifu na vitu vingine kama vyakula n.k, na mambo mengine yanayoathiri ufanisi wa viuatilifu na afya za watumiaji."alisema ndugu Florence


Licha ya haho amewapongeza Washiriki waliofuzu vyema mafunzo hayo lakini pia TPHPA kwa ujumla kwa jitihada zao katika kuhakikisha wanawaelimisha Wakulima na Wafanyabiashara Tanzania nzima ili kuleta tija katika kilimo jambo ambalo ndio ndoto ya serikali yetu na kufikia lengo la agenda 10/30.

Aidha msisitizo ulitolewa na Kaimu Meneja wa Kanda bi.Zuhura Msigwa kwa washiriki wa mafunzo kuwa kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao katika fani hii ya viuatilifu na mabomba waendelee kuwa na mawasiliano ya karibu na wawezeshaji toka TPHPA, Arusha na Kanda pamoja na maeneo mengine wanayotoka ili kuweza kuboresha huduma zao na kukidhi mahitaji ya taifa na wateja wao.

 Akitoa tathmini ya jumla Mratibu wa Mafunzo ndg.Jumanne Rajabu amesema wastani wa jumla wa ufahulu ni asilimia 82 hivyo amewapongeza na kuwataka ambao hawakufuzu kutokata tamaa,aidha amesisitiza kuwa walioajiri au watakaoajiri wafanyakazi katika maduka yao wafanye jitihada za kuwapatia fursa ya kuhudhuria haya mafunzo ya taaluma maalum ya Viuatilifu .  Hii itawasaidia kujikinga na madhara ya Viuatilifu na pia kuwapa wakulima ambao ndio wadau wakubwa wa maduka haya elimu stahiki ya matumizi sahihi ya Viuatilifu kwa udhibiti endelevu wa visumbufu vya mazao.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu