TPHPA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU MKOANI MOROGORO VIWANJA VYA NANENANE KUANZIA LEO TAREHE 2/12/2024 MPAKA TAREHE 7/12/2024














Sasa TPHPA imefika katika mkoa wa Morogoro ikiendelea kutoa mafunzo Ikiwa leo ni siku ya kufungua mafunzo haya ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu mkoani Morogoro katika viwanja vya nanenane jengo la TARI wadau wote mnakaribishwa ikiwa na wauzaji wa viuatilifu, wakulima , Maafisa ugani wa ngazi zote  na  Wataalamu mbalimbali. 

 

Mafunzo haya yamefunguluwa na Meneja kanda ya Mashariki Dr Sasamalo kwa kuwa karibisha washiriki wote waliohudhuria mafunzo haya nakuwahakikishia watatoka wakiwa ni walimu wazuri kwa wengine  na hii itawasaidia wauzaji wa viuatilifu kuwapa wakulima viuatilifu vilivo salama na sahihi hii itasaidia kuwepo kwa usalama wa chakula ambapo wauzaji watatoa kiuatilifu sahihi kwa mkulima.

 

Aidha Meneja Sasamalo amewapongeza washiriki walio toka mikoa ya Songea, Iringa, Katavi, Singida, kuja kushiriki mafunzo haya hapa mkoani Morogoro akawaomba wajitoe kwa nguvu zote katika mafunzo haya na anawakaribisha wale ambao hawajajitokeza hawajachelewa kwani ndiyo mwanzo wa mafunzo.  

 

Vilevile amewahakikishia washiriki Maafisa wawezeshaji kutoka mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania wapo tayari kwaajiri ya kuwapa mafunzo wakulima , Maafisa Ugani wa ngazi zote na wataalamu mbalimbali hivyo wote mnakaribishwa katika viwanja vya nanenane.

 

Aidha Mratibu wa mafunzo ya usimamizi wa viuatilifu  Ndugu Jumanne Rajabu Musalama Akishirikiana na Ndugu Fredy Gabriel alianza kwa kuwapima uelewa washiriki kwa kuwapa jaribio la kukitambua kiuatilifu kupitia maelekezo yaliyowekwa katika kifungashio cha kiuatilifu na kuwapa maelekezo namna ya kusoma maelekezo yaliyopo katika kifungashio na jinsi ya kuvaa wakati wakuhudumia wateja akiwa dukani hata atakae tumia akiwa shambani.

 

 

Hakika wadau wamejitokeza kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Songea, Iringa , Singida, Katavi, na hapahapa Morogoro kutoka Kilosa, Ifakara , Mrimba. Hivyo wakulima wote na wauzaji wa viuatilifu mnakalibishwa katika viwanja hivi vya nanenane ili muweze kupata mafunzo haya ambayo ni muhimu na kwaajiri ya kilimo chenye tija 

 

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu