Wadau wa Mbegu wakutana Arusha kujadili uhusiano kati ya genebanks na mifumo ya mbegu Nchini











TPHPA- Arusha

Leo, Februari 10, 2025, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea TPHPA, Dkt. Sospeter Kabululu, amefungua kikao cha kuimarisha uhusiano wa genebanks na mifumo ya mbegu, kilichofanyika jijini Arusha. Kikao hiki ni sehemu ya mradi wa BOLD (Biodiversity for Opportunities, Livelihoods, and Development), unaofadhiliwa na Serikali ya Norway, na unaolenga kuongeza upatikanaji wa mazao kwa wakulima kupitia genebanks.

Akifungua kikao hicho, Dkt. Kabululu aliwasisitiza washiriki umuhimu wa kuongeza ushirikiano kati ya genebanks na mifumo ya mbegu ya kitaifa. Alisema, "Kuunganisha genebanks na mifumo ya mbegu ni hatua muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na za kutosha, hivyo kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao yetu." 

Kikao hiki kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka mashirika na taasisi zinazoshirikiana na mradi huo, ikiwa ni pamoja na Alliance of Bioversity International and CIAT, PELUM – Tanzania, Sokoine University, TARO, TPHPA, TARI, World Vegetable Centre, TOSCi, ASA, NMBU kutoka Norway, na MVIWARUSHA.

Kikao hiki ni muendelezo wa mkutano wa awali iliyofanyika tarehe 13 Aprili 2023, Dodoma. Ambapo unatoa fursa ya kujadili mikakati ya kuunganisha genebanks na mifumo ya mbegu ya kitaifa ili kuboresha upatikanaji wa mbegu bora.Wadau pia wanajadili mikakati ya kuanzisha miradi ya majaribio kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa mifumo ya mbegu.

Malengo ya kikao ni pamoja na kuelezea na kuthibitisha matokeo ya tathmini na kutoa mrejesho kwa ajili ya kuboresha ripoti, kusikiliza mapendekezo kutoka kwa wadau juu ya kuimarisha ushirikiano na matokeo ya mifumo ya mbegu, kujadili na kutengeneza mikakati ya kuanzisha miradi ya majaribio kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mbegu na vifaa vya kupanda, na kukuza ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na genebank ya taifa, ili kuboresha utendaji wa mfumo wa mbegu wa taifa.Kikao hiki kitamalizika tarehe 12 Februari 2025.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu