KOMGAMANO KANDA YA KASKAZINI KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
![]() |
Akiwa kama mgeni rasmi Waziri Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax amefungua kongamano hilo leo jijini Arusha kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) ambapo agenda kuu ya Kongamano hilo ni "Ushiriki wa Wanawake katika Utalii na Maliasili : Miaka 30 ya Azimio la Beijing.
Akizungumza na Wanawake waliojitokeza kwenye Kongamano hilo Dkt. Stergomena amewaasa wanawake kuwa na uthubutu kujitokeza kwenye majukwaa mbalimbali Kitaifa na Kimataifa yanayohusu shughuli za Kitalii na Maliasili na kuondoa dhana ya kwamba Sekta ya Utalii na Maliasili ni kazi ya wanaume pekee.
"Nimefurahi sana kuwaona Wanawake waliotajwa kuwa ni Wakurugenzi na Wamiliki wa Makampuni mbalimbali ya Kitalii siku hii ya leo na hivyo nawaasa wanawake wengine kuiga na kuwaona wanawake hawa kuwa kama mfano" Dkt Stergomena alisema.
Aidha Kongamano hili limekuwa uwanja wa kuhamasisha jamii kutokomeza vitendo ya ukatili wa kijinsia kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni na badala yake kuwapa nafasi wanawake kwenye fursa mbalimbali za kiuchumi na kisiasa haswa Wasichana ambao wamekuwa na changamoto nyingi kwenye safari yao ya Elimu.
Watumishi Wanawake kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nao hawakubaki nyuma kwenye kuhudhuria Kongamano hili ambalo limehudhuriwa na Wanawake wote wa Kanda ya Kaskazini kujadili namna ambavyo wanaweza kuleta mabadiliko Chanya kwenye sekta ya Utalii na Maliasili.
Comments
Post a Comment