TPHPA KANDA YA MASHARIKI YAJUMUIKA NA WADAU WA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU KURASINI DAR ES SALAAM KATIKA IFTAR GALA








Leo, tarehe 28/3/2025, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Dkt. Mahamudu Sasamalo, amewakaribisha wadau wote waliojumuika na TPHPA katika ofisi za Kurasini, Dar es Salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Prof. Joseph Ndunguru. Lengo ni kuendelea kushirikiana na wadau katika kutekeleza malengo ya taasisi, wizara na serikali kwa ujumla, kuboresha maisha ya Watanzania.

Dkt. Sasamalo alieleza mafanikio ya TPHPA katika utekelezaji wa agenda 10/30, akibainisha ongezeko la mashine za maabara, kama HPLC na GS-MS, ambazo zitachakata sampuli nyingi kwa mwaka. Aidha, alieleza kuwa huduma za TPHPA zimeimarika na kwamba wamefanikiwa kununua ndege kwa ajili ya kudhibiti milipuko ya wadudu waharibifu, hivyo kulinda usalama wa chakula.

Pia, TPHPA inafungua masoko mapya ya mazao kama Pilipili, Parachichi, Mashudu ya Pamba, na Alizeti, na wanajiandaa kufungua masoko ya Karanga, Vanilla, Mahindi meupe, Viungo, na Choroko. Vilevile, tumeandaa nyaraka za kufungua masoko mapya katika nchi 15, na thamani ya mauzo ya nje imepanda kutoka bilioni 1.2 (2021) hadi bilioni 3.5 (2023/24).

Wadau wakiwa ni Katibu Mkuu Croplife Tanzania na wafanyabiashara wa viuatilifu na mazao walipongeza ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya TPHPA na wadau, na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika kukuza sekta ya kilimo nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu