TPHPA Yawajengea Uwezo Mawakala wa Pembejeo za Kilimo na AMCOs zaidi ya 300 Mkoa wa Njombe Kutumia Mfumo wa E-Kilimo
Machi 28, 2025, Wataalamu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Makao Makuu Arusha kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametoa huduma ya kujengea uwezo kwa mawakala wa pembejeo za kilimo na AMCOs zaidi ya 300 kutoka Mkoa wa Njombe kuhusu Mfumo mpya wa kidijitali wa kuomba vibali wa E-Kilimo.
Katika tukio hilo, wafanyabiashara hao wamepata fursa ya kusajili biashara zao na wengine kuhuisha vibali vilivyoisha muda wake. Pia, wamepata mafunzo kuhusu faida za mfumo huu wa kisasa, ambao unarahisisha mchakato wa kuomba vibali na leseni kwa wadau wa kilimo, huku pia ukitoa huduma mbalimbali zinazotolewa na TPHPA.
Mfumo huu wa kisasa utasaidia kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa vibali halali, na hivyo kusaidia kuzuia biashara za viuatilifu zisizo na vibali, kulinda afya ya mimea na mazingira, na kuhakikisha mazao yanakidhi viwango vya ubora kwa soko la ndani na la kimataifa. Aidha, ni takwa la kisheria kwamba ili kufanya biashara ya viuatilifu nchini, wafanyabiashara lazima wawe na kibali halali kutoka TPHPA, hivyo kuhakikisha biashara zao zinakuwa salama na halali.
Comments
Post a Comment