Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi TPHPA wapewa Mafunzo ya Magonjwa Yasiyoambukiza na UKIMWI







Machi 5, 2025 - Mbeya: Afisa Muuguzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Ndugu Yusuph Owanga, kwa kushirikiana na Mratibu wa UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Mkoa wa Mwanza, wameendesha mafunzo maalum kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na UKIMWI kwa Baraza la Wafanyakazi wa TPHPA.


Mafunzo haya, yaliyofanyika katika Hoteli ya Eden Highlands jijini Mbeya, yamelenga kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, pamoja na mbinu bora za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Ndugu Yusuph Owanga alisisitiza umuhimu wa mtindo bora wa maisha, ulaji wa chakula chenye virutubisho vyote, na kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia za msingi za kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza. Aliongeza kuwa uelewa wa wafanyakazi kuhusu UKIMWI unahitajika kuimarishwa ili kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa kikamilifu na kupunguza unyanyapaa dhidi ya waathirika.

Mratibu wa UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Mkoa wa Mwanza naye aliwahimiza washiriki kuendelea kuwa mabalozi wa afya katika jamii zao kwa kusambaza elimu waliyoipata.

Washiriki wa mafunzo haya walieleza kufurahishwa na uhamasishaji huo na kuahidi kutumia maarifa waliyopata kuboresha afya zao na za wenzao mahali pa kazi na katika jamii zao kwa ujumla.

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) inaendelea kujikita katika kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na afya bora ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu