TPHPA YAENDELEA NA ZOEZI LA KUONDOA MAGUGU VAMIZI ZIWA VICTORIA – MWANZA
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kupitia Ofisi yake ya Kanda ya Ziwa chini ya Kaimu Meneja, Bi. Mary Dominick Leina, leo Mei 21, 2025, imeendelea na zoezi la kuondoa magugu vamizi aina ya gugu maji yaliyoenea katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Zoezi hili lilianza rasmi mwezi Februari 2025 na limekuwa likitekelezwa na wataalamu wa Mamlaka kwa kushirikiana kwa karibu na wadau wengine, likiwa na lengo la kudhibiti kuenea kwa gugu hilo hatarishi pamoja na kuchukua sampuli kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina kuhusu athari zake katika mfumo wa ikolojia ya ziwa hilo.
Wataalamu wa TPHPA wamekuwa bega kwa bega na Kamati Maalum iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakishirikiana na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Hadi sasa, utekelezaji wa zoezi hilo unaendelea vizuri huku juhudi zikiendelea kuhakikisha kuwa gugu maji linaondolewa kwa ufanisi na mazingira ya Ziwa Victoria yanarejea katika hali yake ya kawaida.
Comments
Post a Comment