TPHPA YASHIRIKIANA NA PPD ZANZIBAR KUKABILI BAA LA PANYA MASHAMBANI,HEKA 700 ZA MAZAO ZADHIBITIWA KUTOKANA NA PANYA WAHARIBIFU
Katika jitihada za kuimarisha usalama wa chakula na kulinda uzalishaji wa mazao visiwani, TPHPA kwa kushirikiana na Divisheni ya Plant Protection ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo, wanafanya ushirikiano kwa pamoja ya kudhibiti baa la panya kwa kutumia sumu iliyotolewa na TPHPA.
Zoezi hili ni kufuata ombi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa TPHPA, likiwa ni sehemu ya mpango wa haraka kukabiliana na baa la panya waharibifu katika mashamba ya Mpunga yenye kubwa wa heka takriban 700 kwa Unguja na Pemba.
Kupitia ushirikiano huo, TPHPA imepeleka wataalam wake visiwani kwa ajili ya kusimamia zoezi zima la maandalizi, utoaji wa elimu ya namna ya udhibiti kwa wakulima, pamoja na uchanganyaji na usambazaji wa sumu kwa uangalizi wa kitaalamu.
“Huu ni mfano bora wa ushirikiano kati ya taasisi za Muungano. "Tumepokea sumu kutoka TPHPA baada ya kuwasilisha mahitaji yetu, na wamekuja pamoja na wataalamu wao kusimamia na kuhakikisha inatumiwa kwa usalama na kwa ufanisi,” alisema Mkuu wa Divisheni ya Plant Protection Zanzibar Mr. Adam
Wakulima wamefaidika si tu kwa kupata sumu ya kudhibiti panya, bali pia kwa kupata mafunzo kuhusu matumizi salama ya sumu hiyo.
Kwa upande wao, wataalam wa TPHPA walisema ushirikiano huu ni sehemu ya dhamira ya TPHPA kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo nchini kote ili kuhakikisha changamoto za visumbufu zinashughulikiwa kitaalamu na kwa wakati.
Operesheni hii ya pamoja inaonesha namna taasisi za serikali, zinavyoweza kushirikiana kwa ufanisi katika kulinda sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi.
Kwa kushirikiana hivi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo chini ya DPP(Divisheni ya Ulinzi wa mimea) na Wizara ya Kilimo Tanzania Bara kupitia TPHPA wanatoa mfano halisi wa utekelezaji wa sera ya kitaifa ya ushirikiano kati ya sekta, huku pia wakichangia kwa vitendo malengo ya Agenda 10/30, inayolenga kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula kupitia teknolojia na usimamizi bora wa rasilimali.
Comments
Post a Comment