TPHPA YATOA ELIMU KWA WATAALAM WA PPD PEMBA JUU YA MATUMIZI NA USIMAMIZI WA UTEGAJI WA SUMU YA PANYA MASHAMBANI



Pemba – Wataalam kutoka Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wameendesha mafunzo kwa watumishi wa Divisheni ya Plant Protection (PPD) Pemba kuhusu matumizi sahihi na taratibu za usimamizi wa utegaji wa sumu ya panya mashambani.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa pamoja kati ya TPHPA na Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo ili kukabiliana na baa la panya waliokuwa wakisababisha uharibifu katika mashamba ya mpunga yaliyopo maeneo mbalimbali ya Pemba.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bi Christina Tewele  Amewasisitiza umuhimu wa kuzingatia hatua zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya matumizi ya sumu mashambani. Aidha, alifafanua juu ya aina ya sumu inayotumika, vipimo sahihi vya kuchanganya, muda wa kuweka chambo, na mbinu za kutathmini ufanisi wa zoezi la utegaji.

Wakiongea Wataalamu wa PPD wameishukuru TPHPA kwa mafunzo hayo a kuahidi kuwa watatumia elimu hiyo kwa kuhakikisha wanawasimamia wakulima. na kutoa maelekezo ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea na kisha kuokoa mazao yao kutokana na uharibifu  wa panya.

Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo wataalamu hao ili waweze kuwasaidia wakulima katika suala zima la utegaji wa sumu na kuwapa maelekezo jinsi y

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu