WAZIRI BASHE AAGIZA UNUNUZI WA NDEGE TATU ZAIDI KWA AJILI YA UDHIBITI WA VISUMBUFU VYA MIMEA NA MAZAO













Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, ameitaka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kuanza mara moja mchakato wa kununua ndege nyingine tatu za kunyunyuzia viuatilifu ifikapo kabla ya Julai 1, 2025. Agizo hilo amelitoa leo Mei 30, 2025, wakati wa hafla ya mapokezi ya ndege mpya ya kilimo aina ya Thrush 510P2+ iliyofanyika katika Uwanja wa TAA jijini Dodoma.

Mhe. Bashe amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa taifa kukabiliana na milipuko ya visumbufu vinavyoharibu mazao kama Quelea quelea, viwavijeshi vamizi, na nzige, ili kulinda usalama wa chakula na kuongeza tija kwa wakulima.

Ndege hiyo mpya, yenye uwezo wa kubeba lita 1,930 za viuatilifu na kufanya kazi angani kwa zaidi ya saa 4, ni hatua ya mapinduzi katika kilimo cha kisasa. Prof. Joseph Ndunguru, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, amesema ndege hiyo pia itatumika kwa uchunguzi wa kisayansi katika milipuko ya visumbufu nchini. Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wake, Prof. Andrew Temu, imesisitiza dhamira ya kuhakikisha ndege hiyo inatumika kwa ufanisi mkubwa kwa manufaa ya kilimo nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu