TPHPA yashiriki Maonesho ya Nane Nane Morogoro, Yawavutia Wadau kwa Elimu ya Nyoka Anayesaidia Kudhibiti Panya





Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) inashiriki kikamilifu Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane kwa mwaka 2025 mwaka  yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, mkoani Morogoro, kuanzia Agosti 1 hadi 8, 2025. Ushiriki wa TPHPA umejikita katika kutoa elimu kwa wakulima na wadau wa kilimo kuhusu afya ya mimea, matumizi sahihi ya viuatilifu, na mbinu bunifu za kudhibiti visumbufu vya mazao, lakini pia taratibu za usafirishaji mazao nje ya nchi na uingizaji ndani ya nchi. 


Mojawapo ya vivutio vina yo endelea kupata umaarufu mkubwa katika Banda la TPHPA ni maonesho  ya nyoka maalum anayejulikana kwa uwezo wake wa kuwinda na kuua panya mashambani. Nyoka huyo, ambaye hafugwi kama mnyama wa nyumbani bali huonyeshwa kwa lengo la elimu, ameibua mjadala mpana kuhusu njia mbadala zisizotumia sumu katika udhibiti wa panya, ambao ni tatizo kubwa kwa wakulima wengi nchini.


Wadau wa kilimo kutoka maeneo mbalimbali walifurika katika banda hilo wakionesha shauku na kufurahishwa na elimu waliyopata  kuhusu jinsi nyoka huyu anavyosaidia kulinda mazao kwa njia ya asili. Wengi walikiri kutokuwa na uelewa kuhusu mchango wa baadhi ya wanyamapori katika mfumo wa ikolojia wa kilimo, hususan katika kupunguza athari za visumbufu kama panya bila kutumia kemikali.


Kupitia maonyesho haya, TPHPA inatoa elimu ya moja kwa moja, vielelezo halisi, na majaribio ya vitendo, lengo likiwa ni kuwajengea wakulima uelewa wa kina na uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa uzalishaji endelevu wa mazao.


Maonesho ya Nane Nane ni jukwaa muhimu kwa taasisi kama TPHPA kufikia jamii, na mwaka huu, kwa mara nyingine tena, taasisi hiyo imedhihirisha dhamira yake ya kuunga mkono maendeleo ya kilimo salama na chenye tija kwa wakulima wa Tanzania.o

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Apokea Makombe 6 yaliyopatikana Katika Mashindano ya Mei Mosi na SHIMMUTA 2024