Posts

Showing posts from July, 2023

TPHPA na TBC Wakubaliana kufanya Mashirikiano kutoa Elimu kwa Wananchi

Image
  Na Innocent Natai -TPHPA Leo Julai 6, 2023 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA)  Prof. Joseph Ndunguru akiambatana na Wataalamu wa Mamlaka hiyo wamekutana na Kufanya mazungumzo ya Mashirikiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha  Katika ofisi za shirika hilo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es salaam, kwa lengo la kuangalia namna ya kufanya mashirikiano ya kutangaza shughuli zinazofanywa na mamlaka kwa kutoa elimu kutumia vyombo vya habari vilivyopo chini ya shirika hilo. Katika mazungumzo viongozi hao wamekubaliana kufanya mashirikiano katika kuhakikisha wadau wa Afya ya Mimea na Viuatilifu wanapata habari na elimu ili kuendelea kukuza kilimo hapa nchini na Baada ya mazungumzo hayo wamepata fursa ya kutembelea studio mbalimbali za shirika hilo zilizopo Mikocheni.