"Tutaimarisha Masoko ya Mazao yetu kwa kupunguza Viuatilifu vyenye Madhara Makubwa kwa Binadamu na Mzingira" Prof.Kweka

Pichani: Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Eliningaya Kweka(Aliyesimama) akifungua Kikao cha Wataalamu kutoka TPHPA, Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa, Mkemia Mkuu wa Serikali, Mazingira na wadau wengine wa Kilimo na Viuatilifu Leo Juni 22,2023, Hoteli ya Gold Crest -Arusha. Na Innocent Natai - TPHPA Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)kwa kushirikiana na Wataalamu wa Afya na Mazingira wamekutana Leo Juni 22,2023 katika Hoteli ya Gold Crest -Arusha kuandaa mikakati ya kupitia Viuatilifu vyenye madhara makubwa na ya muda mrefu kwa Mazingira na Binadamu vinavyopelekea Matukio ya Watu kutumia Kujiuwa Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Eliningaya Kweka amesema kuwa malengo makubwa ni kuona namna ya kuviondoa viuatilifu hivyo vyenye madhara ya muda mrefu kwa mazingira na Binadamu Hii ni ili kuhakikisha Wakulima wanakuwa Salama na Mazao yanayolimwa Tanzania yanalimwa kwa kutumi...