Posts

Showing posts from December, 2023

Mafuriko Hanang: TPHPA yaunga Mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Image
Na Innocent Natai   Leo Disemba 14,2023 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ameongoza kundi la Viongozi na Watumishi wa Mamlaka hiyo kutembelea na Kutoa Msaada kwa Waathirika wa Maafa ya Mafuriko Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara yaliyotokea Usiku wa kuamkia Disemba 3,2023 na kusababisha uharibifu wa Mali,Vifo na Majeruhi  Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Prof. Ndunguru amesema kuwa Mamlaka hiyo imeguswa na tukio hilo hivyo imekuja kuunga mkono jitihada za  Rais wa  Jamhuri ya Muungano  wa  Tanzania Mhe. Dkt  Samia Suluhu Hassan   katika kuhakikisha waathirika wa Mafuriko Mkoani hapo wanasaidiwa ili waweze kurudi katika hali zao za kawaida, aidha pia ametumia wasaa huo kutoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hilo huku akiwaombea waliopata majeraha kupona haraka na kurejea katika shughuli za kulijenga Taifa Kupitia msaada huo Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatil...

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja aipongeza FAO na TPHPA

Image
Pichani; Bi Gress Matiku ambaye ni Mtaalamu wa kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) akimkabidhi  Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja Mashine ya kupandiia (Planter)  Leo Disemba 2. 2023 Wilaya ya Hanang  Pichani Bi Gress Matiku ambaye ni Mtaalamu wa kudhibiti Visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) akitoa maelezo ya matumizi ya mtego wa kukamata Viwavijeshi kwa  Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja  Na Innocent Natai Kuelekea msimu mpya wa Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja amelipongeza Shirika la Chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa ushirikiano walioufanya na kuwezesha kutoa elimu ya namna ya kudhibiti Visumbufu vya Mimea aina ya Viwavijeshi kwa wakulima Mfano na kutoa Vifaa vya Kilimo na Pembejeo za Kilimo ili kuw...