Prof. Joseph Ndunguru afika Maonesho ya Saba Saba, Atuma ujumbe kwa Wadau

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa Kilimo nchini kutembelea katika katika maonesho ya 48 ya kibiashara ya kimataifa (Saba Saba) Dar es salaam hususani katika banda la TPHPA ili kuweza kupata Elimu na Huduma Mbalimbali Ameyasema hayo leo Julai 10, 2024 wakati alipotembelea katika maonesho hayo katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa TPHPA imeendelea kutoa elimu na huduma kwa wadau nchini ili kuhakikisha wanafikia adha ya Serikali ya kumkomboa Mkulima "Wadau tembeleeni katika banda letu hapa Tent la Katavi mtapata kufahamu masuala mengi kuhusiana taratibu mbalimbali za kufanya biashara za mazao na viuatilifu." amesema Prof. Ndunguru Katika ziara hiyo, Prof.Ndunguru alipata pia nafasi ya kutembelea katika mabanda mengine ya Taasisi na bodi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo Aidha Maonesho haya yalianza Juni 28,2024 na yanayota...