Washiriki Mafunzo ya 62 usimamizi sahihi wa Viuatilifu (pestcide Management) PM2 Watakiwa Kutotanguliza Maslahi Mbele bali wazingatie miiko na taratibu

Mafunzo ya siku 14 ya Usimamizi wa Viuatilifu(Pesticide Management) ya 62(PM2) yamehitimishwa Leo 30/5/2023 katika ofisi za makao makuu ya TPHPA, Ngaramtoni – Arusha, huku washiriki wakikumbushwa kuwa waadilifu na kuhakikisha hawatangulizi maslahi yao mbele katika biashara ya uuzaji wa viuatilifu. Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Mgeni rasmi ndugu Kengese katika kufunga mafunzo hayo aliwasisitiza washiriki kuwa wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa matumizi ya viuatilifu yanafanyika kwa kuzingatia kanuni, maadili ili kulinda afya ya binadamu na kuhakikisha usalama wa chakula pamoja na mazingira bila kuweka maslahi yao binafsi mbele. “Ni muhimu kutambua kuwa taaluma mnayobeba inahusisha uhai wa watu na usalama wa chakula chetu. Msiruhusu maslahi binafsi ya kifedha au ya kibiashara kuwa kikwazo cha kuwajibika kwa uadilifu, mkatoe elimu kwa wakulima ambao ndio wateja wenu kwa usahihi,"alisisitiza ndugu Kengese Mafunzo haya yali...