Posts

Showing posts from September, 2023

KAIMU MKURUGENZI TPHPA PROF.JOSEPH NDUNGURU AMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUWEKA NGUVU KATIKA SEKTA YA KILIMO

Image
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu(TPHPA) Prof.Joseph Ndunguru ametoa pongezi  hizo wakati akifungua  Mkutano wa mwaka wa Tanzania Entomological Association (TEA) uliofanyika New Safari Hotel Arusha ambapo yeye alikuwa Mgeni rasmi. Akizungumza amesema Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr.Samia Suluhu Hassan amejikita katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya  Kilimo na kuhakikisha anaweka nguvu nyingi katika kuhakikisha kilimo kinakuwa na kukuza uchumi wa nchi yetu na si hivyo tu lengo lake ni kuona Tanzania inalisha dunia Jambo ambalo linawezekana wote Kwa pamoja tukiweka juhudi na kufanya kilimo cha kisasa. Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka wanachama hao kukutana mara kwa mara  ili kwa pamoja kujadili changamoto za wadudu waharibifu wanaoleta uharibifu katika mazao ya kilimo na kuja na utatuzi thabiti ili kumaliza tatizo hilo na  kufanya kilimo kiwe chenye tija na kukuza uchumi. Akiongelea suala la kuwawezesha ...

WAFANYAJI SHUGHULI ZINAZOTUMIA VIUATILIFU WATAKIWA KUFANYA UPIMAJI KUGUNDUA MASALIA YA VIUATILIFU KATIKA MIILI YAO UPIMAJI

Image
 Mtaalam wa Maabara kutoka TPHPA Ndg.Raphael Mwezi amewataka wafanyaji shughuli zinazoambatana na matumizi ya Viuatilifu kufanya upimaji ili kubaini kama kuna masalia ya Viuatilifu katika miili yao ili kuwahi mapema matibabu kabla mwilibhaujadhurika zaidi hata kupelekea kifo. Akielezea shughuli za sehemu ya kitengo hicho amesema kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya utumiaji WA Viuatilifu ambapo imekuwa ikipelekea madhara makubwa kwa wahusika akielezea madhara hayo amesema sumu iliyopo kwenye Viuatilifu huingia katika mwili wa binadamu kupitia hewa,midomo,ngozi ambapo sumu ikiingia husambaa katika mfumo WA damu na kuweza kusababisha kifo,ulemavu wa kudumu,saratani ambayo huweza kuja kuonekana baada ya miaka 10-20 ,matatizo ya ini na hata michubuko kwenye mapafu. Katika kuliona hili TPHPA(Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu )wamejikita katika kudhibiti hali hii Kwa njia mbalimbali,Kwanza ni kutoa elimu kwa watumiaji wa Viuatilifu hivi ambapo Mamlaka hukaribisha maombi kupitia bar...

Zoezi la Kudhibiti Kwelea Kwelea Mkoa wa Manyara, Wakulima watuma Ujumbe kwa Uongozi wa TPHPA na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan

Image
Na Innocent Natai    SERIKALI kupitia Mamlaka ya Afya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imefanikiwa kudhibiti Makundi ya Ndege waharibifu aina ya Kwelea Kwelea zaidi ya Milioni 5 na kuokoa zaidi ya Ekari 1000 za zao la mpunga lililolimwa kipindi cha kiangazi  Mkoani Manyara , na kuvamiwa na visumbufu hivyo mwanzoni mwa mwezi Septemba.   Akizungumza wakati wa kukamilisha opeshezani hiyo ya kudhibiti visumbufu hivyo Mtaalamu wa Kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka TPHPA Bwana Gladman Mbukoi amesema zoezi hilo limemaliza kilio cha wakulima wa mpunga kwani kwa siku moja ndege hao walikuwa na uwezo wa kumaliza zaidi ya Tani 50 za zao hilo. Mbukoi amesema katika mkoa huo wamemaliza ndege hao kwa asilimia kubwa na kwamba operesheni hiyo haikuwa nyepesi kutokana na wingi wa ndege hao na kwa siku nne za oparesheni hiyo walikuwa wakifuatilia wanapolala ndege hao na kuwapulizia Vi-uatilifu ili kuwaangamizia wote lengo likiwa kuondolea wakulima usumbufu wa ku...