WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TPHPA WATEMBELEA OFISI ZA TPHPA NAMANGA,WAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Andrew Temu 19 Machi 2024 wametembelea ofisi za Mamlaka zilizopo mpakani mwa Kenya na Tanzania Namanga pamoja na Kituo cha kijasusi cha ukusanyaji wa taarifa za masoko nje ya nchi,lengo likiwa ni kujionea shughuli na changamoto mbalimbali kwa ajili ya kupata ufumbuzi. Akiongea mara baada ya ukaguzi sehemu mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kama vile eneo la ukaguzi,maabara Prof.Andrew Temu amewapongeza kwa namna wanavyofanya kazi kwa kushirikiana na taasisi zingine 18 za serikali zilizopo mpakani hapo lengo likiwa ni kufikia matakwa ya serikali,"Kwa ushirikiano huu niliouona hapa naahidi kuwa balozi wenu nitalisemea hili kila mahali nitakapokwenda aidha nawapongeza sana mamlaka kwa jinsi mnavyochapa kazi katika kuhakikisha sheria zinafuatwa na kuondoa ukiukwaji unaoweza kuleta madhara kwa afya zetu na uchumi wa Tanzania,mna wajibu mkubwa w...