HABARI PICHA:DKT. OSHINGI SHILLA AFUNGUA KIKAO MAALUMU CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TPHPA

Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Usajili na Udhibiti wa Viuatilifu Dkt Oshingi Shilla , akisisitiza jambo wakati akifungua Kikao Maalum cha Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kilichofanyika January 20, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka Hiyo Jijini Arusha . Agenda ya kikao ikiwa ni kujadili bajeti ya Mwaka 2023/2024 ambapo Miongoni mwa vipaumbele vya bajeti ya hiyo ikilenga kulipa mapunjo ya mishahara na madeni ya wafanyakazi (Picha na Innocent Natai) Picha mbalimbali zikionesha wajumbe wa Kikao Maalum cha Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kilichofanyika January 20, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mamlaka Hiyo Jijini Arusha wakichangia ajenda