WASHIRIKI PM2 IRINGA WAELEZWA UMUHIMU WA MAVAZI KINGA ILI KUEPUKA MADHARA

Ikiwa ni siku ya tatu katika mafunzo yanayoendelea kwa Wakulima ,Maafisa kilimo ,wafanyabiashara wa viuatilifu mkoani Iringa Mkufunzi wa Mafunzo ndg.Jumanne amewatahadharisha uzingatiaji wa mavazi kinga wakati wa kutumia viuatilifu ili kuepuka madhara mbalimbali ya muda mrefu na mfupi yanayoweza kutokea iwapo mavazi kinga hayatazingatiwa. Akieleza wakati akifundisha mada hiyo ndg.Jumanne amesema wakulima hawana budi kuzingatia uvaazji wa mavazi yanayotakiwa muda wote wanapotumia viuatilifu ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata kupitia ngozi,pua au katika macho,akikazia hilo ndugu Jumanne amewakumbusha kuwa viuatilifu ni Sumu hivyo kila anaetumia hana budi kujikinga. Akitaja baadhi ya vifaa kinga hivyo vinavyokuwezesha kusaidia viuatilifu visiingie mwilini kupitia sehemu mbalimbali za mwili amesema ni mabuti ya mpira,gloves za mpira,Miwani maalum,vichuja sumu,makoti marefu ya mpira ,kofia