Posts

Showing posts from December, 2024

Tanzania yaanza kupiga hatua mpango wa Usimamizi wa Vifungashio vya Viuatilifu//Wadau wakutana kujadili mikakati

Image
Arusha, Disemba 12, 2024 – Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, amefungua kikao cha wadau kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu jijini Arusha. Kikao hiki kililenga kutafuta suluhu bora ya usimamizi wa vifungashio vya viuatilifu, ili kuhakikisha afya ya binadamu na uhifadhi wa mazingira kwa sasa na katika siku zijazo. Katika hotuba yake, Prof. Ndunguru alisema kwamba kutokuwepo kwa usimamizi mzuri wa vifungashio vya viuatilifu kuna hatarisha mazingira na afya ya binadamu, hasa kwa wakulima wanapotumia viuatilifu bila ya kufuata taratibu bora za usimamizi wa vifungashio hivyo. Bwana Raphael Mwezi, Afisa Mwandamizi kutoka TPHPA, alifafanua kwamba kikao hicho kimejumuisha wadau kutoka sekta mbalimbali, akiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, wakulima, wataalamu kutoka TPHPA, na wadau wa viuatilifu. Lengo kuu la kikao hi...

TPHPA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU MKOANI MOROGORO VIWANJA VYA NANENANE KUANZIA LEO TAREHE 2/12/2024 MPAKA TAREHE 7/12/2024

Image
Sasa TPHPA imefika katika mkoa wa Morogoro ikiendelea kutoa mafunzo Ikiwa leo ni siku ya kufungua mafunzo haya ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu mkoani Morogoro katika viwanja vya nanenane jengo la TARI wadau wote mnakaribishwa ikiwa na wauzaji wa viuatilifu, wakulima , Maafisa ugani wa ngazi zote  na  Wataalamu mbalimbali.     Mafunzo haya yamefunguluwa na Meneja kanda ya Mashariki Dr Sasamalo kwa kuwa karibisha washiriki wote waliohudhuria mafunzo haya nakuwahakikishia watatoka wakiwa ni walimu wazuri kwa wengine  na hii itawasaidia wauzaji wa viuatilifu kuwapa wakulima viuatilifu vilivo salama na sahihi hii itasaidia kuwepo kwa usalama wa chakula ambapo wauzaji watatoa kiuatilifu sahihi kwa mkulima.   Aidha Meneja Sasamalo amewapongeza washiriki walio toka mikoa ya Songea, Iringa, Katavi, Singida, kuja kushiriki mafunzo haya hapa mkoani Morogoro akawaomba wajitoe kwa nguvu zote katika mafunzo haya na anawakaribisha wale ambao hawajajitokeza hawa...

Wakulima wa Mbogamboga, Matunda na Maua Wapata Mafunzo ya Matumizi Sahihi ya Viuatilifu

Image
Arusha, Tanzania 1 Disemba 2024 Wakulima wa mbogamboga, matunda, maua na viungo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamepatiwa mafunzo ya kina kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu katika kilimo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha uzalishaji na uhifadhi wa mazingira. Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili katika Kituo cha TAHA kilichopo Viwanja vya Nanenane, Mkoani Arusha, na yalihusisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya kilimo. Mafunzo hayo yalifadhiliwa na Serikali ya Uholanzi kwa kushirikiana na TPHPA (Tanzania Plant Health and Pesticides Authority) pamoja na TAHA (Tanzania Horticultural Association). Lengo kuu lilikuwa kuwajengea wakulima uwezo wa kutambua na kudhibiti visumbufu mashambani, hasa wadudu na magonjwa, kwa njia salama na endelevu, huku wakizingatia usalama wa mazingira na afya za walaji. Wakulima walifundishwa jinsi ya kutambua visumbufu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wadudu, magonjwa, na kuvu vinavyoathiri mazao yao ya mbogamboga, matunda, maua, na viungo. Pia wali...