Posts

Showing posts from February, 2025

TPHPA Yapokea Ugeni wa Wadau wa FVC, Wakiwemo Mabalozi na Maafisa Kutoka FAO Makao Makuu

Image
Februari 26, 2025, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ilipokea ugeni wa maafisa kumi na mmoja kutoka kwa wadau wa Michango ya Hiari ya Kifedha (FVC). Ujumbe huo ulijumuisha Mabalozi, Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa mjini Roma, Washauri Wakuu kutoka Mashirika ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, pamoja na viongozi wa ngazi za juu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na uliongozwa na Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania, Bi. Nyabenyi Tipo. Katika hotuba yake ya kupokea ugeni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Dkt. Oshingi Shilla, alishukuru kwa ujio wa wadau hao na kueleza jinsi mamlaka na taifa lilivyojivunia misaada inayotokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na FAO Tanzania. Alitaja miradi kama vile Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea na Usalama wa Chakula, ambayo imesaidia kuboresha mifumo ya afya ya mimea na kuimarisha usalama wa chakula nchini Tanzania. "Ushirikiano huu umekuwa na manufaa makubw...

Wataalamu wa TPHPA Wakutana Kujadili Taratibu za Kufungua Masoko ya Nje kwa Zao la Macadamia

Image
Februari 25, 2025, wataalamu kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kutoka idara ya Usimamizi wa Afya ya Mimea walikutana kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kituo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Mimea Kibiolojia, Kibaha. Lengo kuu la kikao hicho kilikuwa kujadili na kuandaa nyaraka za awali zitakazowezesha kufungua masoko ya nje kwa zao la Macadamia. Akizungumza na TPHPA Habari, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Afya ya Mimea, Dkt. Benignus Ngowi, alisema kikao hicho kilijumuisha wataalamu wa masoko ya mazao na afya ya mimea. Waliangazia masuala muhimu kama vile kujua wazalishaji wa zao hilo nchini na kufanya intelijensia kuhusu matakwa ya nchi zinazonunua zao hilo. Kwa upande mwingine, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Malizia Sokoni na Uwezeshaji Biashara, Ndug. Katemani Mdili, alisema mchakato wa kufungua masoko ya nje umeanza kwa haraka kutokana na uhitaji mkubwa wa wakulima wa Tanzania kutaka kusafirisha zao hili kwa ajili ya biashara. Alifafanua kuwa Macadamia ...

TPHPA YASISITIZA UTUNZAJI WA MBEGU ZA ASILI

Image
 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Taifa Cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea (NPGRC) Dkt. Sospeter Mujuni Kabululu wakati alipotembelewa na ugeni wa wataalamu kutoka Lusaka Zambia ambao wametembelea TPHPA kwa ajili ya kujifunza masuala ya namna ya utunzaji na uzalishaji wa mbegu za asili ambapo Kaimu huyo amebainisha kuwa mbegu za asili ni muhimu kutunza kwa ajili ya matumizi ya baadae kwani itasaidia kama akiba ambapo kwa sasa mbegu hizi zimekuwa zikipotea kadri muda unavyozidi kwenda. Akifafanua zaidi Dkt. Kabululu amesema imekuwa ni kawaida kwa jamii ya sasa kutumia mbegu za kununua madukani ambapo kabla hazijaoteshwa zinapitia utafiti wa kimaabara kwa ajili ya chunguzi mbalimbali kuhusu ufanisi wake katika uzalishaji  haswa wa mazao ya chakula na biashara, na kuacha matumizi mbegu za asili kwa mtazamo wa kwamba hazina ufanisi ukilinganisha na mbegu hizo za kisasa. Ameongeza kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nasaba za Mimea haijabaki nyuma kwa kuendelea kutafuta, kuhifadhi na k...

Wadau wa Mbegu wakutana Arusha kujadili uhusiano kati ya genebanks na mifumo ya mbegu Nchini

Image
TPHPA- Arusha Leo, Februari 10, 2025, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea TPHPA, Dkt. Sospeter Kabululu, amefungua kikao cha kuimarisha uhusiano wa genebanks na mifumo ya mbegu, kilichofanyika jijini Arusha. Kikao hiki ni sehemu ya mradi wa BOLD (Biodiversity for Opportunities, Livelihoods, and Development), unaofadhiliwa na Serikali ya Norway, na unaolenga kuongeza upatikanaji wa mazao kwa wakulima kupitia genebanks. Akifungua kikao hicho, Dkt. Kabululu aliwasisitiza washiriki umuhimu wa kuongeza ushirikiano kati ya genebanks na mifumo ya mbegu ya kitaifa. Alisema, "Kuunganisha genebanks na mifumo ya mbegu ni hatua muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na za kutosha, hivyo kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao yetu."  Kikao hiki kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka mashirika na taasisi zinazoshirikiana na mradi huo, ikiwa ni pamoja na Alliance of Bioversity International and CIAT, PELUM – Tanzania, Sokoine University, TARO, TPHPA...