Posts

Showing posts from March, 2025

TPHPA Yawajengea Uwezo Mawakala wa Pembejeo za Kilimo na AMCOs zaidi ya 300 Mkoa wa Njombe Kutumia Mfumo wa E-Kilimo

Image
Machi 28, 2025, Wataalamu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Makao Makuu Arusha kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametoa huduma ya kujengea uwezo kwa mawakala wa pembejeo za kilimo na AMCOs zaidi ya 300 kutoka Mkoa wa Njombe kuhusu Mfumo mpya wa kidijitali wa kuomba vibali wa E-Kilimo. Katika tukio hilo, wafanyabiashara hao wamepata fursa ya kusajili biashara zao na wengine kuhuisha vibali vilivyoisha muda wake. Pia, wamepata mafunzo kuhusu faida za mfumo huu wa kisasa, ambao unarahisisha mchakato wa kuomba vibali na leseni kwa wadau wa kilimo, huku pia ukitoa huduma mbalimbali zinazotolewa na TPHPA. Mfumo huu wa kisasa utasaidia kuongeza ufanisi katika upatikanaji wa vibali halali, na hivyo kusaidia kuzuia biashara za viuatilifu zisizo na vibali, kulinda afya ya mimea na mazingira, na kuhakikisha mazao yanakidhi viwango vya ubora kwa soko la ndani na la kimataifa. Aidha, ni takwa la kisheria kwamba ili kufanya biashara ya viuat...

TPHPA KANDA YA MASHARIKI YAJUMUIKA NA WADAU WA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU KURASINI DAR ES SALAAM KATIKA IFTAR GALA

Image
Leo, tarehe 28/3/2025, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Dkt. Mahamudu Sasamalo, amewakaribisha wadau wote waliojumuika na TPHPA katika ofisi za Kurasini, Dar es Salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Prof. Joseph Ndunguru. Lengo ni kuendelea kushirikiana na wadau katika kutekeleza malengo ya taasisi, wizara na serikali kwa ujumla, kuboresha maisha ya Watanzania. Dkt. Sasamalo alieleza mafanikio ya TPHPA katika utekelezaji wa agenda 10/30, akibainisha ongezeko la mashine za maabara, kama HPLC na GS-MS, ambazo zitachakata sampuli nyingi kwa mwaka. Aidha, alieleza kuwa huduma za TPHPA zimeimarika na kwamba wamefanikiwa kununua ndege kwa ajili ya kudhibiti milipuko ya wadudu waharibifu, hivyo kulinda usalama wa chakula. Pia, TPHPA inafungua masoko mapya ya mazao kama Pilipili, Parachichi, Mashudu ya Pamba, na Alizeti, na wanajiandaa kufungua masoko ya Karanga, Vanilla, Mahindi meupe, Viungo, na Choroko. Vilevile, tumeandaa nyaraka za kufungua masoko mapya katika nchi 15, na thamani ya mauzo ya...

TPHPA yafanya ziara ya kuwajengea uwezo Wafanyabiashara wa Viuatilifu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa namna ya kutumia mfumo wa E- Kilimo

Image
  Wataalamu kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Makao Makuu Arusha, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wameanza ziara ya kujengea uwezo wafanyabiashara wa viuatilifu kuhusu Mfumo mpya wa kidijitali wa kuomba vibali wa E-Kilimo. Ziara hii imeanza rasmi Machi 24, 2025, Mkoani Mbeya na itahusisha mikoa yote inayojumuisha kanda hiyo. Lengo kuu la ziara hii ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa viuatilifu katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni  Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe  ili waweze kujiandikisha na kutumia mfumo wa E-Kilimo kwa urahisi. Mfumo huu unarahisisha mchakato wa kuomba vibali na leseni kwa wadau wa kilimo na kutoa huduma mbalimbali zinazotolewa na TPHPA. Katika ziara hiyo Wafanyabiashara watajengewa uelewa kuhusu faida za mfumo huu wa kisasa, ambao utaongeza ufanisi katika upatikanaji wa vibali halali na kusaidia kuzuia biashara za viuatilifu zisizo na vibali, hivyo kulinda afya ya mimea, mazingi...

TPHPA YAFANYA UKAGUZI KATIKA MASHAMBA MAKUBWA KANDA YA KASKAZINI, WAKULIMA WAFURAHIA UKAGUZI

Image
Wataalam kutoka Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)wapo Kanda ya Kaskazini katika Ziara ya ukaguzi kwenye mashamba makubwa mbalimbali ya mazao yasafirishwayo nje ya nchi  ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za kuhakikisha uzalishaji wa mazao unafuata viwango vya ubora na usalama kwa soko la ndani na kimataifa. Ziara hii inahusisha Ukaguzi wa matumizi ya viuatilifu, udhibiti wa wadudu waharibifu, mifumo ya umwagiliaji, mbinu bora za kilimo na utoaji ushauri katika changamoto wanazokutana nazo wakulima ikiwepo magonjwa yanayoikumba mimea . Katika ziara hii, wataalam wanatembelea mashamba makubwa ya wakulima takriban 25 wanaosafirisha bidhaa zao nje ya nchi ambapo wanashuhudia maendeleo makubwa yaliyotokana na ushauri wa kitaalam unaotolewa na TPHPA. Akizungumza kuhusu  Ukaguzi huu Mtaalam wa TPHPA ndugu Jumanne Mgana amesema malengo ya ukaguzi  katika mashamba hayo ni kukagua mimea na uwepo wa visumbufu vya Karantini na magonjwa yanayoweza kusababisha atha...

TPHPA yawakutanisha wadau Dodoma kuthibitisha Mkakati wa Taifa wa Udhibiti wa Ugonjwa wa Fungashada ya Migomba

Image
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa ushirikiano na Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), kupitia mradi wa STREHIT,Machi 13, 2025 imewakutanisha wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa Mesuma Hoteli, Dodoma, ili kupitia, kujadili, kutoa mapendekezo, na kuthibitisha Mkakati wa Taifa wa Udhibiti wa Ugonjwa wa Fungashada ya Migomba (BBTV). Mkutano huu ulifunguliwa na Ndugu Musa Chidinda, Kaimu  Meneja wa Usimamizi wa Usafi wa Mimea na Karantini ya Taifa(TPHPA)  akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Ndunguru. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano, Ndugu Musa Chidinda alisema, "Ugonjwa wa Fungashada ya Migomba ni tishio kwa uzalishaji wa ndizi nchini, zao ambalo ni muhimu kwa lishe, kipato cha wakulima, na uchumi wa taifa kwa ujumla. Serikali kupitia TPHPA imechukua hatua madhubuti kuhakikisha tunapambana na ugonjwa huu kwa njia mbalimbali, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wakulima, uangamizaji wa migomba iliyoathirika, n...

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi TPHPA wapewa Mafunzo ya Magonjwa Yasiyoambukiza na UKIMWI

Image
Machi 5, 2025 - Mbeya: Afisa Muuguzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Ndugu Yusuph Owanga, kwa kushirikiana na Mratibu wa UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza wa Mkoa wa Mwanza, wameendesha mafunzo maalum kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na UKIMWI kwa Baraza la Wafanyakazi wa TPHPA. Mafunzo haya, yaliyofanyika katika Hoteli ya Eden Highlands jijini Mbeya, yamelenga kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya moyo, pamoja na mbinu bora za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Ndugu Yusuph Owanga alisisitiza umuhimu wa mtindo bora wa maisha, ulaji wa chakula chenye virutubisho vyote, na kufanya mazoezi mara kwa mara kama njia za msingi za kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza. Aliongeza kuwa uelewa wa wafanyakazi kuhusu UKIMWI unahitajika kuimarishwa ili kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa kikamilifu na kupunguza unyanyapaa dhidi ya waathirika. Mratibu wa UKIMWI...

Mafunzo ya Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Awamu ya Nne yafunguliwa rasmi na Prof. Joseph Ndunguru

Image
Machi 6, 2025 k atika Hoteli ya Eden Highlands, Mbeya  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, amefungua rasmi mafunzo ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Awamu ya Nne (2023-2030). Mafunzo haya, yaliyohudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Uadilifu na viongozi wa Mamlaka  ambao ni sehemu ya menejimenti , yanalenga kuhakikisha kuwa viongozi wa TPHPA wanapata uelewa wa kina kuhusu mbinu bora za kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwajibikaji, uadilifu, na usimamizi bora wa rasilimali ndani ya TPHPA. Pia, mafunzo haya yanahimiza viongozi wa Mamlaka kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuhakikisha mifumo ya uwazi inaimarishwa ili kutoa huduma bora kwa wakulima na wadau wa sekta ya kilimo.  Katika hotuba yake, Prof. Ndunguru alisisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya uwazi na uwajibikaji ndani ya Mamlaka ili kutoa huduma bora kwa wakulima na wadau wa kilimo. A...

KOMGAMANO KANDA YA KASKAZINI KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Image
Akiwa kama mgeni rasmi Waziri Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax amefungua kongamano hilo leo jijini Arusha kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) ambapo agenda kuu ya Kongamano hilo ni "Ushiriki wa Wanawake katika Utalii na Maliasili : Miaka 30 ya Azimio la Beijing. Akizungumza na Wanawake waliojitokeza kwenye Kongamano hilo Dkt. Stergomena amewaasa wanawake kuwa na uthubutu kujitokeza kwenye majukwaa mbalimbali Kitaifa na Kimataifa yanayohusu shughuli za Kitalii na Maliasili na kuondoa dhana ya kwamba Sekta ya Utalii na Maliasili ni kazi ya wanaume pekee. "Nimefurahi sana kuwaona Wanawake waliotajwa kuwa ni Wakurugenzi na Wamiliki wa Makampuni mbalimbali ya Kitalii siku hii ya leo na hivyo nawaasa wanawake wengine kuiga na kuwaona wanawake hawa kuwa kama mfano" Dkt Stergomena alisema. Aidha Kongamano hili limekuwa uwanja wa kuhamasisha jamii kutokomeza vitendo ya ukatili wa kijinsia kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni na badala y...