TPHPA yaanza mpango wa kibaiolojia Kunusuru Ziwa Victoria Dhidi ya Gugu Maji

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kupitia maabara zake za kisasa zilizopo katika Kituo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Mimea Kibiolojia, Kibaha, mkoani Pwani, imeanza kuzalisha mdudu rafiki wa mazingira aina ya "mbawa kavu" (Cyrtobagous salviniae) kwa ajili ya kudhibiti gugu maji vamizi (Salvinia molesta). Gugu hilo limekuwa tatizo kubwa katika Ziwa Victoria na vyanzo vingine vya maji hapa nchini, likisababisha athari kwa usafiri, mazingira, uchumi na maisha ya jamii zinazotegemea ziwa hilo. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa zoezi hilo, tarehe 18 Julai 2025, Mkurugenzu wa Usalama wa Afya ya Mimea TPHPA, Dkt. Benignus Ngowi, amesema matumizi ya mdudu rafiki huyo ni sehemu ya mkakati endelevu wa kutumia mbinu za kibaiolojia kudhibiti visumbufu bila kuathiri mazingira. Alibainisha kuwa njia hiyo ni salama, rafiki kwa viumbe hai wengine na inaweza kusaidia kupunguza gharama kubwa zinazotumika katika kudhibiti magugu hayo. Kwa upande wake, Ndugu Keneth Nyakung...