Posts

Showing posts from August, 2024

MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU YANAYOTOLEWA NA TPHPA NI CHACHU YA AGENDA 10/30

Image
Katibu Tawala msaidizi wa Mkoa wa Mbeya (Kitengo cha Uchumi na Uzalishaji) Ndg.Said Juma ambae alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Matumizi sahihi na salama ya viuatilifu Mkoani Mbeya 30/8/2024 yanayotolewa na TPHPA amesema mafunzo haya  yatasaidia sekta ya kilimo katika kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye Agenda 10/30,hivyo mafunzo haya ni muhimu na ni chachu ya kufikia lengo hilo la agenda 10/30 na TPHPA ni wadau muhimu katika kufanikisha matokeo chanya ya kilimo nchini hususani ya agenda 10/30. Akitahadharisha juu ya athari mbalimbali zinazotokana na ulaji wa vyakua ambavyo vimenyunyizwa viuatilifu kwa njia isiyo sahihi na salama ndg.Said amesema watu wote tunaingia kwenye kupata madhara wakiwepo wao wakulima na wafanyabiashara  hivyo amewataka kila mhitimu akawe balozi mzuri wa matumizi sahihi na salama ya viuatilifu  ili kuepuka madhara hayo. Pamoja na hayo amewasihi na kuwataka washiriki wa Mafunzo wakatoe elimu ya matumizi sahihi na salama ya Viuat...

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Apongeza TPHPA kwa Mchango Mkubwa Katika Usalama wa Chakula

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli, ametoa pongezi kwa Uongozi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa juhudi zake za kipekee katika kudhibiti visumbufu vya mazao vinavyokabili wakulima wa Wilaya hiyo. Akizungumza na Waandishi wa Habari na Maafisa wa kitengo cha habari na Mawasiliano TPHPA leo, Agosti 29, 2024 katika ofisi zake, Mhe. Nguli alisema Mamlaka hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa wakulima wa Wilaya hiyo kwa kupambana na visumbufu vya mazao kabla havijaleta athari kubwa kwa mazao, jambo linalopelekea usalama wa chakula na ongezeko la mazao. “Huduma za kudhibiti visumbufu zilikuwa zinatolewa mara moja kwa mwaka, lakini tangu kuanzishwa kwa mamlaka hii, huduma hizo sasa zinatolewa mara mbili kwa misimu. Hii ni hatua muhimu katika kuongeza uzalishaji wa mazao na kuchangia katika usalama wa chakula wilayani Mvomero,” alieleza Mhe. Nguli. Aidha, Mhe. Nguli alitoa shukrani kwa TPHPA kwa huduma nzuri zinazotolewa kwa haraka wanapohitajika katika Wilay...

TPHPA Yatunukiwa Tuzo ya Kipekee kwa Mchango wa Kiuchumi na Kijamii

Image
  Arusha, 28 Agosti 2024 Katika tukio la kihistoria lililofanyika mapema leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ilipokea heshima kubwa kwa kutunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwa kutambua mchango wake mkubwa kiuchumi na kijamii. Tuzo hizi hutolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa taasisi ambazo zimeonyesha juhudi za kipekee katika kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Mamlaka hii imeonyesha ufanisi wa hali ya juu katika kudhibiti balaa la panya, ambapo imeweza kutatua changamoto hiyo katika mikoa 16, wilaya 54, kata 540, na vijiji 1,395. Juhudi hizi zimesaidia wakulima wapatao 58,886 kwa kuokoa jumla ya ekari 895 za mazao yao, hivyo kuimarisha usalama wa chakula na kuleta athari chanya kwa uchumi wa nchi. Pia, TPHPA ilifanya kazi kubwa katika kudhibiti ndege aina ya kwelea kwelea, ambapo zaidi ya ndege milioni 80 waliovamia mazao katika...

Naibu Waziri wa Kilimo,Mhe.David Silinde afanya ziara Kituo cha Ukaguzi cha Mamlaka Namanga//atoa Maelekezo kwa Wakaguzi

Image
                                           Leo, Agosti 16, 2024, Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa David Silinde, alifanya ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa katika Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) kilichoko Namanga, mkoani Arusha. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Silinde aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mheshimiwa Marko Henry Ng'umbi, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, pamoja na viongozi wengine wa Mamlaka hiyo. Katika ofisi za Ukaguzi za Mamlaka, Mheshimiwa Silinde alitoa pongezi kwa kazi zinazofanywa na wakaguzi wa Mamlaka waliopo katika ofisi hizo, akisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi. Alisema kuwa, shughuli hizo ni muhimu sana kwa kuhakikisha kwamba bidhaa zinazopita katika Mpaka huo zinafuata viwango vilivyowekwa, hivyo kusaidia nchi kuepuka kuingiza visumbufu na kuharibu masoko kwa ...

TPHPA Kwa kushirikiana na taasisi zingine yaanza Mikakati kupunguza Vifo vinavyotokana na Viuatilifu

Image
Katika warsha iliyohudhuriwa na washiriki kutoka Mamlaka na Taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali iliyofanyika tarehe 13 mpaka 14 Agosti 2024, Hapa Mkoani Arusha washiriki waliweza kujadiliana na kupata mafunzo ya kutumia programu iitwayo “KoboCollection Programu hii yenye kufanya kazi maalumu ya kuhifadhi taarifa za Idadi ya Vifo vilivyotokana na kujiua kwa kutumia Viuatilifu ambapo taarifa hizo zitatumika na Mamlaka za Usalama na Afya ya Mimea kufahamu ni sumu au viuatilifu gani vinatumiwa na watu wanaotaka kujiua, umri wao, mahala pa tukio na taarifa zingine muhimu. Wawakilishi kutoka vyombo vya Usalama, Wizara ya Afya, Kilimo na Mamlaka za Mazingira waliongozwa na Mwezeshaji kutoka Shirika lisilo la Kiserikali kutoka Kenya (CEJAD) Ndg. Fredrick Otieno ambapo alisema mradi huo utasaidia kuondoa changamoto hiyo ikiwa vyombo husika vitatoa ushirikiano kwani vifo vya kujiua kwa kutumia viuatilifu vinazidi kuongezeka. Pia aliongeza kwa kuelezea baadhi ya njia zitakazo...