Posts

Showing posts from October, 2023

WATAALAM TPHPA WATAKIWA KUTUMIA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KONGWE MWITU(SANSEVIERIA) KUPATA TAALUMA NA MBINU ZA UTAFITI WA MMEA HUO

Image
Na Mariam Makombe -TPHPA Hayo yamejiri katika kongamano la Kimataifa la SANSEVERIA linalofanyika katika ukumbi wa TPHPA ambapo Mgeni rasmi Dkt.Sospeter Kabululu akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Prof.Joseph Ndunguru  amewata wataalam wanaoshiriki kutumia fursa hiyo kujifunza Kwa umakini mbinu mbalimbali zinazotumika katika kutafiti mmea wa Kongwemwitu ambao una maajabu mengi na faida kubwa kwa binadamu na mustakabali wa dunia kwa ujumla. Akiongea mara baada ya kufungua Kongamano hilo amesema mkutano huu umekusanya Watafiti mbalimbali kutoka ujerumani,ufaransa,Uganda,Kenya, Zanzibar n.k ambapo kwa pamoja wanajadili kuhusu mmea huu wa Kongwemwitu ( Sansevieria) na kuona ni namna gani mikakati ifanyike katika kuhifadhi mmea huu wa kipekee  ambao uko katika aina tofauti zaidi ya Mia moja  usipotee katika uso wa dunia kutokana na shughuli za binadamu. "Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu moja ya jukumu letu ni kuhifadhi mimea nasi tunabeba jukumu kuhakikisha mmea h...

KEMI Waahidi kuendeleza Mashirikiano na TPHPA //Wafanya ziara Kujionea Shughuli zinazofanywa na Mamlaka

Image
 KEMI (Swedish chemical agency) kutoka Sweden ambao pia ni washirika wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu (TPHPA) kwa muongo mmoja sasa wametembelea ofisi za Mamlaka kwa nia ya kujifunza masuala mbalimbali ya Mamlaka hii haswa katika maswala ya udhibiti wa viuatilifu. Akizungumza Mwakilishi Kaimu Mkurugenzi Ndg.Osmund Ndomba wakati akiwakaribisha wageni hao ambao wamekuwa wakitekeleza miradi kwa pamoja na TPHPA amesema wamefurahishwa na ujio wao katika ofisi za TPHPA ambapo pamoja na shukran hizo amewashukuru pia KEMI kwa kuwawezesha kupata mafunzo  juu ya masuala ya Viuatilifu watumishi takribani 13 wa Mamlaka ambapo ujuzi huo utasaidia Sana katika kuelimisha jamii ya wakulima juu ya matumizi bora ya Viuatilifu kwa ajili ya usalama wa Afya ya mimea,aidha amezungumzia juu ya changamoto ya asilimia kubwa ya wakulima kutojua taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuata katika kufanya biashara za mazao kimataifa ambapo Mamlaka imekuwa ikifanya juhudi Kuwaelimisha kwa kutoa elimu...

Kuelekea Msimu mpya wa Kilimo Wilaya ya Hanang TPHPA na FAO wajitosa kunusuru matumizi makubwa ya rasilimali wakati wa uzalishaji

Image
Na Innocent Natai Kuelekea msimu mpya Mpya wa Kilimo Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) wametoa elimu ya namna ya kudhibiti Visumbufu vya Mimea aina ya Viwavijeshi Kwa wakulima Mfano Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara ili kuwasaidia kuepukana na athari za matumizi makubwa ya rasilimali fedha na muda wakati wa kupambana na visumbufu hivyo. Akizungumza baada ya Mafunzo hayo  Bi Gress Matiku ambaye ni mtaalamu wa kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) amesema kuwa mafunzo hayo yamejumuisha wakulima Ishirini na Tano (25) na Maafisa Ugani kutoka Kata mbalimbali za Wilaya hiyo na dhumuni la mafunzo hayo ikiwa ni kutoa elimu ya udhibiti Shirikishi ya kudhibiti Viwavijeshi Vamizi. Amesema kuwa mafunzo hayo yamejumuisha elimu ya kuchagua mbegu bora,kumtambua viwavijeshi, hatua sahihi ya kumdhibiti, Kutambua viuatilifu sahihi vya kumdhibiti na m...

HAFLA YA MAKABIDHIANO VIFAA VYA UBORESHAJI AFYA YA MIMEA YAFANA, KAIMU MKURUGENZI ABAINISHA MANUFAA YATAKAYOPATIKANA,AMTAJA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)imepokea msaada wa vifaa wenye thamani ya Bil.2.2 kutoka FAO 10/10/2023 ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mh.David Silinde. Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Prof.Joseph Ndunguru pamoja na kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kuwa mistari wa mbele kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo Kwa lengo la kuongeza ajira,kutanua masoko na hata kuiongezea Bajeti Wizara ya kilimo Pia  amebainisha mafanikio yatakayopatikana kutokana na vifaa hivyo ambapo amesema vifaa hivyo vitadaidia katika kuongeza maduhuli ya Serikali Kwa maana ya kuongeza mapato kutokana na ufanisi utakaoongezeka kutokana na vifaa hivyo kurahisisha utendaji wa kazi ambapo upande wa magari yatasaidia katika ufuatiliaji katika katika ukaguzi ,aidha vifaa vitasaidia katika kudhibiti na uhakika wa chakula na malighafi ya viwanda,mbali na Hilo vitasaidia kugundua visumbufu vi...

TPHPA yazidi kusonga mbele Zoezi la Udhibiti wa Panya waharibifu Mkoa wa Morogoro //Wakulima wapongeza

Image
  Na Innocent Natai    SERIKALI kupitia Mamlaka ya Afya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Ekari  931,920 Mkoani Morogoro zilizovamiwa na Panya waharibifu na kuziwezesha Kaya 1682 kuwa na uhakika wa kupata mavuno na usalama wa mavuno yao baada ya kuyatoa shambani.   Akizungumza wakati wakiendelea na zoezi hilo lililoanza Septemba 23,2023  Kaimu Mkuu wa Kituo cha kudhibiti Baa la Panya TPHPA ( Morogoro) Bi.  Christina Tewele  amesema zoezi hilo linaendelea vizuri na wapo ukingoni kulitamatisha kwa kuhakikisha wanadhibiti mlipuko huo wa Panya waharibifu ili kuwasaidia wakulima kuepukana na upotevu wa mazao yao kabala na baada ya mavuno Amesema Mamlaka hiyo imefanya kazi ya udhibiti wa panya hao kwa awamu Mbili (2) mwezi Agosti na Septemba na  Jumla ya kata zoezi hilo lilipofanyika ni Nane (8) na Jumla ya vijiji Ishirini na Mbili (22) vyenye jumla ya kaya zilizochanga chambo 1682 vimehudumiwa. "chambo kilichochangwa...