Posts

Showing posts from September, 2024

TPHPA Yafanikisha kuandaa Nyaraka za Ufunguo wa Masoko Mapya kwa Mazao ya Kipaumbele Tanzania

Image
TPHPA- Dodoma Katika hatua muhimu kwa maendeleo ya kilimo nchini, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa Msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU), kupitia mradi wa kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea na Usalama wa Chakula, wamefanikiwa kuandaa nyaraka za ufikiaji wa masoko kwa mazao 8 ya kipaumbele katika nchi 14. Hafla ya uzinduzi ilifanyika tarehe 18 Septemba 2024 katika Ukumbi wa Morena Hoteli Jijini Dodoma, ikiwa na mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde. Katika hafla hiyo, Mhe. Silinde alikabidhi nyaraka za ufunguzi wa masoko kwa Bw. Salvatory Mbilinyi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Nyaraka hizi zinalenga kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa mazao, ambayo kwa sasa bado hayajafikiwa kutokana na masharti ya awali yanayohitajika. Mazao yanayohusika ni pamoja na vanilla, nanasi, parachichi, pilipili manga, kakao, na tumbaku, yanayot...

Jumla ya washiriki 82 wamehitimu mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu Kanda ya Nyanda za juu Kusini.

Image
    Jumla ya washiriki 82 wamehitimu mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu Kanda ya  Nyanda za juu Kusini. Washiriki hao wameishukuru Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA), kwa kuwaongezea uelewa zaidi na wameahidi kuwa watahakikisha wanaenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo. Akifunga mafunzo hayo Afisa Kilimo Mkoa wa Njombe ndug. Wilson Joel amesema, kipimo kwa washiriki baada ya mafunzo hayo ni namna watavyoweza kupunguza malalamiko ya wakulima na kuthibiti visumbufu. Aidha, amewasisitiza wafanyabiashara wa viuatilifu kuajiri watu waliopatiwa mafunzo hayo ili waweze kutoa huduma iliyosahihi. Bwana Wilson amesema, mafunzo hayo yanalenga moja kwa moja afya za watu hivyo washiriki hao wakatekeleze yote waliyofundishwa. Mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu Kanda ya Nyanda za juu kusini yamefungwa rasmi Septemba 14 Makambako Mkoani Njombe

Wakulima Waonywa Kuhusu Matumizi yasiyosahihi ya Viuatilifu

Image
TPHPA - NJOMBE Katika mafunzo yanayoendelea kuhusu matumizi sahihi na salama ya viuatilifu yanayofanyika Makambako, Mkoani Njombe, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewaonya watumiaji wa viuatilifu dhidi ya tabia ya kuzidisha au kupunguza vipimo vya viuatilifu katika kunyunyuzia mazao yao. Bwana Christian Mayige, Mkufunzi wa mafunzo haya kutoka TPHPA, alisisitiza umuhimu wa kufuata maagizo sahihi kuhusu vipimo vya viuatilifu. Katika mafunzo yake, Mayige alieleza kwamba baadhi ya wakulima wanajitahidi kuzidisha vipimo vya viuatilifu kwa dhana ya kudhibiti visumbufu kwa haraka, lakini hii inaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu. "Wakulima wengi wanapenda kuzidisha vipimo vya viuatilifu wakiamini kuwa hivi ndivyo wataweza kudhibiti visumbufu kwa haraka," alisema Mayige. "Hata hivyo, hatua hii ina hatari ya kuacha viuatilifu vingi kwenye mazao, jambo ambalo si salama kwa mwanadamu." Katika mafunzo hayo, Mayige alitoa mwongozo kuhusu matumizi sahi...

TPHPA yazidi kuwanoa Maafisa wake katika Matumzi ya TEHAMA, Dkt. Oshingi Shilla Afungua Mafunzo ya Siku Mbili

Image
TPHPA - MWANZA Leo, Septemba 12, 2024, katika Ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Buzuruga, Jijini Mwanza, Dkt. Oshingi Shilla, akimwakilisha   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), ameongoza ufunguzi wa mafunzo muhimu ya siku mbili kuhusu Mfumo wa e-board.   Mfumo wa e-board ni teknolojia ya kisasa iliyokusudia kuboresha na kuharakisha uratibu wa shughuli za uandaaji vikao vya bodi na menejimenti katika Taasisi na Mamlaka za Umma. Mfumo huu unasaidia katika kuandaa yatokanayo kwenye kikao, kupiga kura, na kutengeneza ripoti za utendaji kazi katika vipindi mbalimbali vya mwaka.   Katika hotuba yake, Dkt. Shilla alisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi na uwazi katika usimamizi wa vikao. Alieleza kuwa Mfumo wa e-board unalenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za bodi na menejimenti kwa kuzingatia ufanisi na uharaka, huku ukifanikisha uratibu mzuri na uwezeshaji wa kazi kwa wahusika wote. Mafunzo ...

Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Afungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi - Mwanza

Image
                                           TPHPA- MWANZA Leo, Septemba 10, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, amefungua rasmi kikao cha siku moja cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Jijini Mwanza Katika hafla hiyo, Prof. Ndunguru alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya wafanyakazi na uongozi ili kuimarisha utendaji na kuongeza ufanisi katika sekta ya afya ya mimea na viuatilifu. Alibainisha kuwa kikao hiki ni fursa muhimu kwa wafanyakazi kutoa maoni, kujadili changamoto, na kupanga mikakati ya kuboresha huduma na mazingira ya kazi. Kikao hicho kilihudhuriwa na Menejimenti, Wakuu wa Vitengo na Kanda, wawakilishi kutoka Vitengo mbalimbali vya Mamlaka, pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka. Wakati wa kikao, masuala kadhaa muhimu yaliyojadiliwa ni ...